NB-Picha haihusiani na habari hapa chini
Wakazi wa Kijiji cha Ivaini Kenya wamejawa na hofu baada ya nyumba ya mzee mmoja kuteketezwa kwa moto na viumbe visivyoonekana ambapo ishu hiyo inahusishwa na imani za kishirikina.
Mzee huyo Mukai Kimanzi amesema nyumba yake iliteketezwa na majini yanayoiandama familia yake na yamekuwa yakimkosesha usingizi, yanamtia hofu kwa kuwapiga makofi  wakiwa usingizini.
“Waliniambia waliona moto tu unachoma kila kitu kwa kweli nyumba.. moja imechomeka na nyingine bado zinachomeka, kulingana vile mimi naona, mimi naona ni mapepo tu” Mzee Mukai Kimanzi.
Majirani wa eneo hilo wamesema nyumba hiyo imeteketezwa na mapepo mabaya na kudai kuwa huwa hali inakuwa tofauti inapotimia saa moja usiku, yeyote atakaesogea eneo hilo anarushiwa mawe na majini hayo.
Mzee huyo amelazimika kuondoka nyumbani kwake na kuishi kwa ndugu yake ambae nae anataka kumfukuza mzee huyo kutokana na hofu kwamba atavamiwa na majini hayo.

Facebook Blogger Plugin by AllyTz

Chapisha Maoni

 
Top